Sunday, February 1, 2015
UFUNUO WA YOHANA
Ufunuo wa Yohana
1
Utangulizi:
Kitabu hiki kinaanza, “Ufunuo wa Yesu Kristo aliopewa na Mungu… “ kikionyesha kuwa Yesu Kristo ndiye mhusika mkuu katika kitabu hiki. Tangu mwanzo kuonekana kwa Kristo ndiko kunakotawala. Hivyo Ufunuo huu ni wa Yesu Kristo aliopewa na Mungu, japo kitabu kimechukua jina la mwandishi, “Ufunuo wa Yohana”, ukweli ni kwamba haumzungumzii Yohana kwa undani wala haumfunui yeye, bali Yesu Kristo. Yesu ndiye Mwana Kondoo ambaye ameleta ukombozi. Yeye ndiye atakayehukumu na hatimaye atashinda kabisa uovu, ili ufalme wa milele ulio bora kabisa usimamishwe.
Kuna sehemu kubwa tatu katika kitabu hiki chenye mambo mengi muhimu. Sehemu ya kwanza ni maono ya Yesu Kristo, (sura ya 1). Sehemu ya pili inahusu habari za makanisa, yaani, barua zinazoandikwa kwa makanisa saba yaliyoko Asia (sura ya 2-3). Sehemu ya tatu inahusu maono mbalimbali juu ya maisha na mateso ya watu wa Mungu, kushindwa kwa uovu, kuja kwa Kristo mara ya pili, hukumu ya mwisho, utawala wa miaka elfu moja na maisha ya mbinguni ( sura ya 4-22). Sehemu kubwa ya maono hayo inahusu maafa yatakayoipata dunia ambapo ghadhabu ya Mwana-Kondoo, yaani, Yesu, inaonyeshwa. Katika maono haya yamo pia maono kuhusu watu wa Mungu walioteswa na kuuawa ambao sasa wako mbinguni. Maono yanafikia kilele kwenye vita baina ya yule kahaba Babeli na ushindi wa Neno la Mungu ambaye ni Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana (19:16). Yeye amekuja kuangamiza kazi za Shetani (uovu) na kuandaa karamu kwa wale wamwaminio. Ndipo yanafuata maono kuhusu hukumu na utukufu na maneno ya mwisho, ‘Amen, na uje Bwana Yesu’ (22:20).
Mstari wa ufunguo wa kitabu hiki ni (1:19 “Basi andika mambo uliyoyaona, yaliyoko na yale yatakayotukia baada ya haya.” Kikiwa na lugha ya kiufunuo, yaani, matumizi ya mifano na majina ya kubuniwa ambayo si halisi, lugha ya mfano, ndoto, maono, matumizi makubwa ya tarakimu na viumbe vya mbinguni. Tumaini kwa wale wanaoteswa katika nyakati zile za kukata tamaa.
Wazo Kuu
Kitabu hiki chenye utukufu kinamwonyesha Yesu ambaye mwanzo alidharauliwa, Mwana-Kondoo aliyechinjwa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu, akichukua utawala wa historia nyakati za mwisho na akileta ushindi wa milele kwa kuangamiza uovu na kuleta utawala wa haki milele na milele. Mkristo katika kitabu hiki anapata uhakika wa tumaini lake kwamba: siku moja mambo yote yatakuwa mema na Mungu atatawala juu ya yote. Machozi yatafutwa, kifo, huzuni, majonzi na uchungu vitakoma milele’’ (21:4). Huu ni ujumbe wa kutia moyo kwa waamini wote, wakati wote.
Mwandishi
Yale yaliyomo kwenye kitabu hiki na ushahidi wa nje unaonyesha kwamba mwandishi ni mtu aliyekuwa na nafasi muhimu ya uongozi katika makanisa ya Asia. Mwandishi wa kitabu hiki ni Yohana, ‘‘Mimi Yohana, ndugu yenu ninayeshiriki pamoja nanyi mateso katika Yesu… ‘’, (1:9-10), ambaye ametajwa mahali pengi (1:1, 4, 9: 21:2 na 22:8). Huyu ndiye aliyeandika pia Injili pamoja na nyaraka zote tatu, ambaye ndiye yule anayetajwa kama mwanafunzi aliyependwa na ambaye aliegama kifuani mwa Yesu wakati wa chakula cha mwisho kati ya Yesu na wanafunzi Wake.
Tarehe
Kitabu hiki kimeandikwa 96 B.K.
Mahali
Kisiwa cha Patmo karibu na pwani ya Uyunani (Greece).
Mgawanyo
•
Mwanzo wa maono (1:1-20)
•
Barua saba kwa Makanisa (2:1-3:22)
•
Maono kuhusu Mungu na
Mwana-Kondoo (4:1-5:14)
•
Lakiri saba za hukumu (6:1-8:5)
•
Tarumbeta saba za hukumu (8:6-11:19)
•
Maono kuhusu vita ya duniani na
mbinguni (12:1-14:20)
•
Mabakuli saba ya hukumu (15:1-16:21)
•
Hukumu juu ya Kahaba Babeli ( 17:1-19:21)
•
Mwisho wa nyakati na wakati ujao ( 20:1-22:21)
Ufunuo wa Yohana
2
Utangulizi Na Salamu Ufunuo wa Yesu Kristo aliopewa na Mungu ili awaonyeshe watumishi Wake mambo yatakayotukia karibuni. Alijulisha mambo haya kwa kumtuma malaika Wake kwa Yohana mtumishi Wake, 2ambaye ameshuhudia kuhusu kila kitu alichoona, yaani, Neno la Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo. 3Amebarikiwa yeye asomaye maneno ya unabii huu na pia wamebarikiwa wale wanaoyasikia na kuyatia moyoni yale yaliyoandikwa humo, kwa sababu wakati umekaribia.
Salamu Kwa Makanisa Saba
4Yohana,
kwa makanisa saba yaliyoko Asia:
Neema na amani kutoka kwa Yeye aliyeko, aliyekuwako na atakayekuja na kutoka kwa wale Roho saba walioko mbele ya kiti Chake cha enzi 5na kwa Yesu Kristo ambaye ni shahidi mwaminifu, aliye mzaliwa wa kwanza kutoka kwa wafu, ambaye Yeye ndiye mtawala wa wafalme wa dunia.
Kwake Yeye aliyetupenda na ambaye ametuweka huru kutoka katika dhambi zetu kwa damu Yake, 6akatufanya sisi kuwa ufalme na makuhani, tumtumikie Mungu Wake ambaye ni Baba yake. Utukufu na uwezo vina Yeye milele na milele! Amen.
7Tazama! Anakuja na mawingu
na kila jicho litamwona,
hata wale waliomchoma mkuki,
na mataifa yote ulimwenguni
yataomboleza kwa sababu yake.
Naam ndivyo itakavyokuwa! Amen.
8‘‘Mimi ni Alfa na Omega,’’ asema Bwana Mungu, ‘‘Aliyeko, aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.’’
Maono Ya Kristo
9Mimi Yohana, ndugu yenu ninayeshiriki pamoja nanyi mateso katika Yesu na katika ufalme na uvumilivu katika saburi, nilikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo kwa ajili ya neno la Mungu na ushuhuda wa Yesu. 10Nilikuwa katika Roho siku ya Bwana, nikasikia sauti kubwa kama ya tarumbeta nyuma yangu 11ikisema, “Andika kwenye kitabu haya yote unayoyaona, kisha ukipeleke kwa makanisa saba, yaani: Efeso, Smirna, Pergamo, Thiatira, Sardi, Filadelfia na Laodikia.’’
12Ndipo nikageuka ili nione ni sauti ya nani iliyokuwa ikisema nami. Nami nilipogeuka, nikaona vinara saba vya taa vya dhahabu, 13katikati ya vile vinara vya taa, nikaona mtu kama Mwana wa Adamu, amevaa joho refu na mkanda wa dhahabu umefungwa kifuani mwake. 14Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu, nyeupe kama theluji, nayo macho yake yalikuwa kama mwali wa moto. 15Nyayo zake zilikuwa kama shaba iliyosuguliwa sana, kama vile imesafishwa katika tanuru ya moto, nayo sauti yake ilikuwa kama sauti ya maji mengi. 16Katika mkono wake wa kuume alishikilia nyota saba na kinywani mwake ulitoka upanga wenye makali kuwili. Uso wake kama jua kali linalong’aa kwa nguvu zake zote.
17Nilipomwona, nilianguka miguuni pake kama aliyekufa. Ndipo akaweka mkono wake wa kuume juu yangu na kusema, “Usiogope, Mimi ni wa Kwanza na wa Mwisho. 18Mimi ni Yeye aliye hai, niliyekuwa nimekufa na tazama, ni hai milele na milele! Nami ninazo funguo za mauti na kuzimua. 19Basi andika mambo uliyoyaona, yaliyopo na yale yatakayotukia baada ya haya. 20Kuhusu siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono Wangu wa kuume na vile vinara saba vya taa vya dhahabu ni hii: zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba, navyo vile vinara saba ni hayo makanisa saba. Kwa Kanisa Lililoko Efeso
‘‘Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika:
Haya ndiyo maneno ya yule aliyezishika zile nyota saba katika mkono wake wa kuume, na ambaye hutembea katikati ya vile vinara saba vya taa vya dhahabu. 2‘‘Nayajua matendo yako, bidii yako na saburi yako. Najua kuwa huwezi kuvumiliana na watu waovu na ya kwamba umewajaribu wale wanaojifanya kuwa mitume na kumbe sio, nawe umewatambua
a18 “Kuzimu” hapa linatokana na neno la Kiyunani “Hades” au
“Tartarus”, yaani, mahali pa mateso kwa ajili ya waliopotea.
1 2
Ufunuo wa Yohana
3
kuwa ni waongo. 3Nami najua umevumilia na kustahimili taabu kwa ajili ya Jina langu, wala hukuchoka.
4Lakini nina neno juu yako: umeuacha upendo wako wa kwanza. 5Kumbuka basi ni wapi ulikoanguka! Tubu na ukafanye matendo yale ya kwanza. Kama usipotubu, nitakuja kwako na kukiondoa kinara chako cha taa kutoka mahali pake. 6Lakini una jambo hili kwa upande wako: unayachukia matendo ya Wanikolai, ambayo nami nayachukia.
7Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho ayaambia makanisa. Yeye atakayeshinda, nitampa haki ya kula matunda ya mti wa uzima, ambao uko katika paradisoa ya Mungu.
Kwa Kanisa Liliko Smirna
8‘‘Kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika:
Haya ndiyo maneno yake Yeye aliye wa Kwanza na wa Mwisho, aliyekufa kisha akafufuka. 9Naijua dhiki yako na umaskini wako, lakini wewe ni tajiri! Nayajua masingizio ya wale wasemao kuwa ni Wayahudi lakini sio, wao ni sinagogi la Shetani. 10Usiogope mateso yatakayokupata. Nakuambia Shetani atawatia baadhi yenu gerezani ili kuwajaribu, nanyi mtapata dhiki kwa muda wa siku kumi. Uwe mwaminifu, hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.
11Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatadhuriwa na mauti ya pili.
Kwa Kanisa Lililoko Pergamo
12‘‘Kwa malaika wa Kanisa lililoko Pergamo andika:
Haya ndiyo maneno yake Yeye aliye na upanga wenye makali kuwili. 13Ninajua unakoishi, ni kule ambako Shetani ana kiti chake cha enzi. Lakini umelishika jina langu. Wala hukuikana imani yako kwangu hata katika siku za shahidi wangu mwaminifu Antipa, ambaye aliuawa katika mji wenu, ambako ndiko anakokaa Shetani.
14Lakini nina mambo machache dhidi yako: unao watu wafuatao mafundisho ya
a7 Paradiso hapa ina maana ya bustani, yaani,shamba dogo la miti
izaayo matunda.
Balaamu, yule aliyemfundisha Balaki kuwashawishi Waisraeli watende dhambi kwa kula vitu vilivyotolewa dhabihu kwa sanamu na kufanya uasherati. 15Vivyo hivyo unao wale wayashikao mafundisho ya Wanikolai. 16Basi tubuni! ama sivyo, nitakuja kwako upesi na kupigana na watu hao kwa upanga wa kinywa changu.
17Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa yeye jiwe jeupe ambalo juu yake limeandikwa jina jipya asilolijua mtu, isipokuwa yule anayelipokea.
Kwa Kanisa Lililoko Thiatira
18‘‘Kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika :
Haya ndiyo maneno ya Mwana wa Mungu, ambaye macho yake ni kama mwali wa moto na ambaye miguu yake ni kama shaba iliyosuguliwa sana. 19Nayajua matendo yako, upendo wako, imani yako, huduma na saburi yako na kwamba matendo yako ya sasa yamezidi yale ya kwanza.
20Lakini nina neno dhidi yako: unamvumilia yule mwanamke Yezebeli ambaye anajiita nabii, lakini anawafundisha na kuwapotosha watumishi wangu ili wafanye uasherati na kula vyakula vilivyotolewa kafara kwa sanamu. 21Nimempa muda ili atubie uasherati wake, lakini hataki. 22Kwa hiyo nitamtupa kwenye kitanda cha mateso, nami nitawafanya hao wanaozini naye kupata mateso makali wasipotubia njia zake. 23Nami nitawaua watoto wake. Nayo makanisa yote yatajua kwamba Mimi ndiye nichunguzaye mioyo na nia za watu na kwamba nitamlipa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake. 24Basi nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, ninyi ambao hamyafuati mafundisho ya Yezebeli, wala hamkujifunza hayo wengine wanayoyaita mambo ya ndani sana ya Shetani (sitaweka mzigo mwingine wo wote juu yenu): 25Lakini shikeni sana mlicho nacho, mpaka nitakapokuja.
26Atakayeshinda na kutenda mapenzi Yangu mpaka mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa.
Ufunuo wa Yohana
4
27‘Atawatawala kwa fimbo ya chuma,
atawavunja vipande vipande kama
chombo cha udongo,
kama vile mimi nilivyopokea mamlaka kutoka kwa Baba yangu. 28Yeye ashindaye nitampa ile nyota ya asubuhi. 29Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho anayaambia makanisa. Kwa‘‘Kwa malaika wa Kanisa lililoko Sardi andika:
Kanisa Lililoko Sardi
Haya ndiyo maneno Yake Yeye aliye na zile Roho saba za Mungu na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, kwamba una sifa ya kuwa hai, lakini umekufa. 2Amka! Nawe uyaimarishe yale yaliyo karibu kufa, kwa maana sikuona kwamba kazi zako zimekamilika machoni pa Mungu wangu. 3Kumbuka basi yale uliyoyapokea na kuyasikia, yatii na ukatubu. Lakini usipoamka, nitakuja kama mwivi wala hutajua saa nitakayokuja kwako.
4Lakini bado una watu wachache katika Sardi ambao hawajayachafua mavazi yao. Wao wataenda pamoja nami, wakiwa wamevaa mavazi meupe, kwa maana wanastahili. 5Yeye ashindaye atavikwa vazi jeupe kama wao, nami sitafuta jina lake kutoka katika kitabu cha uzima, bali nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu na mbele za malaika Wake. 6Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho anayaambia makanisa.
Kwa Kanisa Lililoko Filadelfia
7‘‘Kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika :
Haya ndiyo maneno Yake Yeye aliye mtakatifu na wa kweli, Yeye aliye na ufunguo wa Daudi. Anachokifungua hakuna awezaye kukifunga, wala anachokifunga hakuna awezaye kukifungua. 8Nayajua matendo yako. Tazama, nimeweka mbele yako mlango uliofunguliwa, wala hakuna awezaye kuufunga. Ninajua kwamba una nguvu kidogo lakini umelishika neno Langu wala hukulikana Jina langu. 9Nitawafanya wale wa sinagogi la Shetani, wale ambao husema kuwa ni Wayahudi lakini sio, bali ni
waongo, waje wapige magoti miguuni pako, nao watajua ya kwamba nimekupenda. 10Kwa kuwa umelishika neno la saburi Yangu nitakulinda hata utoke katika saa ya kujaribiwa inayokuja ulimwenguni pote ili kuwajaribu wote wakaao duniani.
11Ninakuja upesi. Shika sana ulicho nacho, ili mtu asije akaichukua taji yako. 12Yeye ashindaye nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo kamwe. Nitaandika juu yake Jina la Mungu wangu na jina la mji wa Mungu wangu, yaani, Yerusalemu mpya, ambao unashuka kutoka mbinguni kwa Mungu wangu. Nami pia nitaandika juu yake Jina langu jipya. 13Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho anayaambia makanisa.
Kwa Kanisa Lililoko Laodikia
14‘‘Kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika :
Haya ndiyo maneno Yake Yeye aliye Amen, shahidi mwaminifu na wa kweli, mtawala wa uumbaji wote wa Mungu. 15Nayajua matendo yako, ya kwamba wewe si baridi wala si moto. Afadhali ungelikuwa baridi au moto. 16 Hivyo kwa kuwa u uvuguvugu, kwamba wewe si baridi wala si moto, nitakutapika utoke kinywani Mwangu. 17Kwa maana unasema, ‘Mimi ni tajiri, nimefanikiwa, wala sihitaji kitu cho chote.’ Hujui ya kwamba wewe ni mnyonge, wa kuhurumiwa, masikini, kipofu, tena uliye uchi. 18Kwa hiyo nakushauri ununue kutoka Kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto ili upate kuwa tajiri na mavazi meupe ili uyavae, upate kuficha aibu ya uchi wako na mafuta ya kupaka macho yako ili upate kuona .
19Wale niwapendao, ninawakemea na kuwaadibisha. Hivyo uwe na bidii ukatubu. 20Tazama, nasimama mlangoni nabisha. Kama mtu ye yote akisikia sauti Yangu na kufungua mlango, nitaingia ndani na kula pamoja naye,naye pamoja nami.
21Yeye ashindaye nitampa haki ya kuketi pamoja Nami kwenye kiti Changu cha enzi, kama vile Mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba Yangu kwenye kiti Chake cha enzi. 22Yeya aliye na sikio na asikie yale
ambayo Roho anayaambia makanisa.’’
3
Ufunuo wa Yohana
5
Kiti Cha Enzi Kilichoko Mbinguni Baada ya mambo hayo nilitazama, nami nikaona mbele yangu mlango uliowazi mbinguni. Nayo ile sauti niliyokuwa nimeisikia hapo kwanza ikisema nami kama tarumbeta ikasema, “Njoo panda huku nami nitakuonyesha yale ambayo hayana budi kutokea baada ya haya.’’ 2Ghafula nilikuwa katika Roho, hapo mbele yangu kilikuwapo kiti cha enzi mbinguni, kikiwa kimekaliwa na mtu mmoja. 3Yeye aliyekuwa amekikalia alikuwa anaonekana kama yaspi na akiki. Kukizunguka kile kiti cha enzi palikuwa na upinde wa mvua ulioonekana kama zumaridi. 4Pia kukizunguka hicho kiti cha enzi palikuwa na viti ishirini na vinne na juu ya hivyo viti walikuwa wameketi wazee ishirini na wanne, waliovaa majoho meupe, wakiwa na taji za dhahabu vichwani mwao. 5Kwenye kile kiti cha enzi palikuwa panatoka miali ya umeme wa radi, ngurumo na sauti za radi. Mbele ya hicho kiti cha enzi, palikuwa na taa saba zilizokuwa zinawaka. Hizi ndizo Roho saba za Mungu. 6Pia mbele ya hicho kiti cha enzi palikuwa na kile kilichoonekana kama bahari ya kioo, iliyokuwa angavu kama jiwe lisilo na rangi yo yote ling’aalo sana.
Katikati, kukizunguka kile kiti cha enzi, kulikuwa na viumbe wanne wenye uhai, wakiwa wamejawa na macho mbele na nyuma. 7Huyo kiumbe wa kwanza mwenye uhai alikuwa kama simba, wa pili alikuwa kama ng'ombe dume, wa tatu alikuwa na uso kama wa mwanadamu na wa nne alikuwa kama tai anayeruka. 8Kila mmoja wa hawa viumbe wenye uhai wanne, alikuwa na mabawa sita na kujawa na macho pande zote, hadi chini ya mabawa. Usiku na mchana hawakuacha kusema:
‘‘Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
ni Bwana Mungu Mwenyezi,
aliyekuwako, aliyeko na atakayekuja.’’
9Kila mara viumbe hao wenye uhai wanne walipomtukuza, kumheshimu na kumshukuru Yeye aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi, tena aishie milele na milele, 10wale wazee ishirini na wanne huanguka mbele Zake Yeye aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi na kumwabudu Yeye aliye hai milele na milele. Wao huziweka taji zao mbele ya hicho kiti cha enzi wakisema,
11“Bwana wetu na Mungu wetu,
Wewe umestahili kupokea utukufu na
heshima na uweza,
kwa maana ndiwe uliyeviumba vitu vyote
na kwa mapenzi Yako viliumbwa
na vimekuwako.’’
Kitabu Na Mwana-Kondoo Kisha nikaona katika mkono Wake wa kuume yule aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi, kitabu kilichoandikwa ndani na upande wa nyuma kikiwa kimefungwa kwa lakiri saba. 2Nami nikamwona malaika mwenye nguvu akitangaza kwa sauti kuu, akisema, “Ni nani anayestahili kuzivunja hizo lakiri na kukifungua hicho kitabu?” 3Lakini hapakuwa na ye yote mbinguni wala duniani au chini ya dunia aliyeweza kukifungua hicho kitabu wala hata kutazama ndani yake. 4Nikalia sana sana kwa sababu hakuonekana ye yote aliyestashili kukifungua hicho kitabu wala kutazama ndani yake. 5Kisha, mmoja wa wale wazee akaniambia, “Usilie! Tazama, Simba wa kabila la Yuda, wa uzao wa Daudi, ameshinda, ili kwamba aweze kukifungua hicho kitabu na kuvunja hizo lakiri zake saba.’’
6Ndipo nikaona kati ya kile kiti cha enzi na wale viumbe wenye uhai wanne na miongoni mwa wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, akiwa kama amechinjwa. Alikuwa na pembe saba na macho saba, ambazo ndizo zile Roho saba za Mungu zilizotumwa duniani pote. 7Huyo Mwana-Kondoo akaja na kukitwaa kile kitabu kutoka kwenye mkono wa kuume wa yule aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi. 8Alipokwisha kukitwaa kile kitabu, wale viumbe wenye uhai wanne pamoja na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele ya yule Mwana-Kondoo. Kila mmoja wao alikuwa na kinubi, nao walikuwa wameshika mabakuli ya dhahabu yaliyojaa uvumba, ambayo ni maombi ya watakatifu. 9Nao wakaimba wimbo mpya wakisema:
“Wewe unastahili kukitwaa kitabu
na kuzivunja lakiri zake,
kwa sababu ulichinjwa
na kwa damu Yako ukamnunulia Mungu
watu
kutoka katika kila kabila, kila lugha,
kila jamaa na kila taifa.
10Wewe umewafanya hawa wawe ufalme na
makuhani wa kumtumikia Mungu wetu,
nao watamiliki katika dunia.’’
4 5
Ufunuo wa Yohana
6
11Nami nikatazama, nikasikia sauti za malaika wengi wakiwa wamekizunguka kile kiti cha enzi, pamoja na wale viumbe wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne, idadi yao ilikuwa kumi elfu mara kumi elfu na maelfu ya maelfu. 12Nao wakiimba kwa sauti kuu, wakisema:
‘‘Anastahili Mwana-Kondoo, Yeye
aliyechinjwa,
kupokea uweza na utajiri na hekima
na nguvu
na heshima na utukufu na sifa!’’
13Kisha nikasikia kila kiumbe mbinguni na duniani, chini ya nchi na baharini na vyote vilivyomo ndani yake vikiimba:
‘‘Sifa na heshima na utukufu na uweza ni
vyake Yeye aketiye juu ya hicho kiti
cha enzi na kwa Mwana-Kondoo,
milele na milele!”
14Wale viumbe wenye uhai wanne wakasema, “Amen!’’ Nao wale wazee ishirini na wanne wakaanguka kifudifudi wakaabudu.
Mwana- Kondoo Avunja Lakiri Saba Kisha nikamwona Mwana-Kondoo akivunja ile lakiri ya kwanza miongoni mwa zile saba. Ndipo nikasikia mmoja wa wale viumbe wenye uhai wanne akisema kwa sauti kama ya radi: “Njoo!’’ 2Nikatazama na hapo mbele yangu alikuwepo farasi mweupe! Yeye aliyempanda alikuwa na upindi, naye akapewa taji, akampanda akatoka akishinda ili apate kushinda.
3Alipoivunja ile lakiri ya pili, nikamsikia yule kiumbe mwenye uhai wa pili akisema, “Njoo!’’ 4Ndipo akatokea farasi mwingine wa rangi nyekundu. Yeye aliyempanda akapewa uwezo wa kuondoa amani duniani na kuwafanya watu wauane. Yeye akapewa upanga mkubwa.
5Alipoivunja ile lakiri ya tatu, nikamsikia yule kiumbe wa tatu mwenye uhai akisema, “Njoo!’’ Nikatazama na mbele yangu alikuwepo farasi mweusi! Yeye aliyempanda alikuwa na mizani mkononi mwake. 6Ndipo nikasikia kile kilichokuwa kama sauti katikati ya wale viumbe wanne wenye uhai ikisema, “Kipimo kimoja cha ngano kwa mshahara wa kibarua wa siku moja. Vipimo vitatu vya shayiri kwa mshahara wa kibarua wa siku mojaa. Lakini usiharibu mafuta ya zeituni wala divai!’’
7Alipovunja ile lakiri ya nne, nikasikia sauti ya yule kiumbe wa nne mwenye uhai ikisema, ‘‘Njoo!’’ 8Nikatazama na hapo mbele yangu alikuwepo farasi mwenye rangi ya kijivujivu! Yeye aliyempanda huyo farasi aliitwa Mauti, naye Kuzimub alikuwa akifuatana naye, nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya dunia, kuua kwa upanga, njaa, tauni na kwa wanyama wakali wa dunia.
9Alipoivunja ile lakiri ya tano, nikaona chini ya madhabahu, roho za wale waliouawa kwa ajili ya Neno la Mungu na kwa ajili ya ushuhuda walioutunza. 10Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, ‘‘Hata lini, Ee Bwana Mwenyezi, uliye Mtakatifu na Mwaminifu, kutokuwahukumu na kulipiza kisasi juu ya watu waishio duniani kwa ajili ya damu yetu?’’ 11Kisha kila mmoja wao akapewa joho jeupe, nao wakaambiwa wangoje kwa muda kidogo zaidi, mpaka idadi ya ndugu zao na watumishi wenzao watakaouawa kama wao walivyouawa, itakapotimia.
12Nikaangalia, Naye alipokuwa akiivunja ile lakiri ya sita, pakatokea tetemeko kuu la nchi na jua likawa jeusi kama nguo ya gunia iliyotengenezwa kwa singa za mbuzi, mwezi wote ukawa mwekundu kama damu. 13Nyota zilizo angani zikaanguka ardhini kama vile matunda ya mtini yasiyokomaa yaangukavyo wakati mti wake unapotikiswa na upepo mkali. 14Anga ikatoweka kama vile karatasi isokotwavyo na kila mlima na kila kisiwa kikaondolewa mahali pake.
15Ndipo wafalme wa duniani, wakuu wote, majemadari, matajiri, wenye nguvu na kila mtu, mtumwa na mtu huru, wakajificha katika mapango na kwenye miamba ya milima. 16Wakaiita milima na miamba wakisema, “Tuangukieni, mkatufiche na uso Wake Yeye aketiye kwenye kiti cha enzi na mkatuepushe na ghadhabu ya Mwana-Kondoo, 17kwa maana siku ile kuu ya ghadhabu yao imewadia.Je, ni nani awezaye kusimama?’’
Wale Wasraeli 144,000 Watiwa Muhuri Baada ya haya nikaona malaika wanne wakiwa wamesimama katika pembe nne za dunia, wakizuia hizo pepo nne za dunia, ili
a6 Mshahara wa kibarua wa siku moja ulikuwa sawa na dinari
moja.
b7 Kuzimu hapa ni neno linalotokana na neno la Kiyunani
“Hades” au kwa Kiebrania “Sheol”
6 7
Ufunuo wa Yohana
7
kwamba pasiwe na upepo utakaovuma juu ya nchi au juu ya bahari au juu ya mti wo wote. 2Nikaona malaika mwingine akipanda kutoka maawio ya jua akiwa na muhuri wa Mungu aliye hai. Akawaita kwa sauti kubwa wale malaika wanne waliokuwa wamepewa mamlaka ya kuidhuru nchi na bahari, akisema, 3“Msiidhuru nchi wala bahari, wala miti, hadi tuwe tumetia alama kwenye vipaji vya nyuso za watumishi wa Mungu wetu.’’ 4Ndipo nikasikia idadi ya wale waliowekewa alama, yaani, watu 144,000 kutoka katika makabila yote ya Israeli.
5Kutoka kabila la Yuda 12,000,
kabila la Reubeni 12,000,
kabila la Gadi 12,000,
6kabila la Asheri 12,000,
kabila la Naftali 12,000,
kabila la Manase 12,000,
7kabila la Simeoni 12,000,
kabila la Lawi 12,000,
kabila la Isakari 12,000,
8kabila la Zabuloni 12,000,
kabila la Yosefu 12,000
na kabila la Benyamini 12,000.
Umati Mkubwa Wa Watu Kutoka Mataifa yote
9Baada ya haya nikatazama na hapo mbele yangu palikuwa na umati mkubwa wa watu ambao hakuna ye yote awezaye kuuhesabu. Kutoka kila taifa, kila kabila, kila jamaa na kila lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi na mbele ya Mwana-Kondoo. Walikuwa wamevaa mavazi meupe na wakiwa wameshika matawi ya mitende mikononi mwao. 10Nao walikuwa wakipiga kelele kwa sauti kubwa wakisema:
“Wokovu una Mungu wetu,
Yeye aketiye kwenye kiti cha enzi
na Mwana-Kondoo!’’
11Nao malaika wote walikuwa wamesimama kukizunguka kile kiti cha enzi na wale wazee ishirini na wanne na wale viumbe wanne wenye uhai. Wakaanguka kifudifudi mbele ya hicho kiti cha enzi na kumwabudu Mungu, 12wakisema:
‘‘Amen!
Sifa na utukufu
na hekima na shukrani na heshima
na uweza na nguvu
viwe kwa Mungu wetu milele na milele,
Amen!’’
13Kisha mmoja wa wale wazee ishirini na wanne akaniuliza, ‘‘Ni nani hawa waliovaa mavazi meupe, nao wametoka wapi?’’
14Nikamjibu, “Bwana, wewe wajua.’’
Naye akasema, “Hawa ni wale waliotoka katika ile dhiki kuu, nao wamefua mavazi yao katika damu ya Mwana-Kondoo na kuyafanya meupe kabisa. 15Kwa hiyo,
“wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu na
kumtumikia usiku na mchana katika
Hekalu Lake,
naye aketiye katika kile kiti cha enzi
atakaa pamoja nao na kuwalinda.
16Kamwe hawataona njaa wala kiu tena.
Jua halitawapiga
wala joto lo lote liunguzalo.
17Kwa maana Mwana-Kondoo aliyeko katikati ya
kile kiti cha enzi atakuwa Mchungaji
wao,
naye atawaongoza kwenda kwenye
chemchemi za maji yaliyo hai.
Naye Mungu atafuta kila chozi kutoka katika
macho yao.’’
Lakiri Ya Saba Na Chetezo Cha Dhahabu Mwana-Kondoo alipoivunja ile lakiri ya saba, pakawa kimya mbinguni kwa muda wa nusu saa.
2Nami nikawaona wale malaika saba wanaosimama mbele za Mungu, nao wakapewa tarumbeta saba.
3Malaika mwingine aliyekuwa na chetezo cha dhahabu, akaja na kusimama mbele ya madhabahu. Akapewa uvumba mwingi ili autoe pamoja na maombi ya Watakatifu wote, juu ya ile madhabahu ya dhahabu iliyoko mbele ya kile kiti cha enzi. 4Ule moshi wa uvumba pamoja na yale maombi ya watakatifu, vikapanda juu mbele za Mungu, kutoka mkononi mwa huyo malaika. 5Kisha yule malaika akachukua kile chetezo, akakijaza moto kutoka kwenye ile madhabahu, akautupa juu ya dunia. Pakatokea sauti za radi, ngurumo, umeme wa radi na tetemeko la nchi.
TARUMBETA SABA
Tarumbeta Ya Kwanza
6Basi wale malaika saba waliokuwa na zile tarumbeta saba wakajiandaa kuzipiga.
7Malaika wa kwanza akaipiga tarumbeta 8
Ufunuo wa Yohana
8
yake, pakatokea mvua ya mawe na moto uliochanganyika na damu, vikatupwa kwa nguvu juu ya nchi na theluthi ya dunia ikateketea, theluthi ya miti ikateketea na majani yote mabichi yakateketea.
Tarumbeta Ya Pili
8Malaika wa pili akaipiga tarumbeta yake na kitu kama mlima mkubwa unaowaka moto kikatupwa baharini. Theluthi ya bahari ikawa damu, 9theluthi ya viumbe vyenye uhai viishivyo baharini vikafa na theluthi ya meli zikaharibiwa.
Tarumbeta Ya Tatu
10Malaika wa tatu akaipiga tarumbeta yake na nyota kubwa iliyokuwa ikiwaka kama taa, ikaanguka toka angani, ikaangukia theluthi ya mito na chemchemi za maji. 11Nyota hiyo inaitwa “Uchungu.’’ Theluthi ya maji yakawa machungu na watu wengi wakafa kutokana na maji hayo kwa maana yalikuwa machungu.
Tarumbeta Ya Nne
12Kisha malaika wa nne akaipiga tarumbeta yake na theluthi ya jua, theluthi ya mwezi na theluthi ya nyota, zikapigwa. Kwa hiyo theluthi moja ya mwanga ikawa giza. Theluthi ya mchana ikawa haina mwanga na pia theluthi ya usiku.
13Nilipokuwa tena nikitazama, nikamsikia tai mmoja akipiga kelele kwa sauti kuu wakati akiruka katikati ya mbingu, akisema, “Ole, Ole, Ole, wa watu waishio duniani, kwa sababu ya tarumbeta ambazo malaika wengine watatu wanakaribia kuzipiga.’’
Tarumbeta Ya Tano Malaika wa tano akaipiga tarumbeta yake, nami nikaona nyota iliyokuwa imeanguka toka angani hadi ardhini. Nyota hiyo ilipewa ufunguo wa shimo lisilo na mwishoa. 2Alipolifungua hilo shimo lisilo na mwisho, moshi ukapanda kutoka humo kama moshi wa tanuru kubwa sana. Jua na anga vikatiwa giza na ule moshi uliotoka katika hilo shimo lisilokuwa na mwisho. 3Ndipo katika ule moshi wakatoka nzige wakaenda juu ya nchi, nao wakapewa nguvu kama zile za nge wa duniani. 4Wakaambiwa wasidhuru majani ya nchi, wala mmea wala mti wo wote, bali wawadhuru tu wale watu ambao hawana alama ya Mungu
a1 Shimo lisilo na mwisho, yaani, “Abyss”maana yake kuzimu
(makao ya pepo wachafu.) kwenye vipaji vya nyuso zao. 5Wakaruhusiwa kuwatesa kwa muda wa miezi mitano, lakini wasiwaue. Uchungu wa kuuma kwao ulikuwa kama ule wa mtu aumwapo na nge. 6Katika siku hizo watu watatafuta kifo lakini hawatakiona, watatamani kufa, lakini kifo kitawakimbia.
7Wale nzige walikuwa na umbo kama la farasi waliotayarishwa kwa ajili ya vita. Kwenye vichwa vyao kulikuwa na kitu kama taji za dhahabu na nyuso zao zilikuwa kama za binadamu. 8Walikuwa na nywele kama za wanawake na meno yao yalikuwa kama ya simba. 9Walikuwa na dirii kama za chuma na sauti za mabawa yao zilikuwa kama ngurumo za magari mengi ya farasi wanaokimbilia vitani. 10Walikuwa na mikia yenye miiba ya kuumia kama nge. Nguvu yao ya kutesa watu kwa huo muda wa miezi mitano ilikuwa katika hiyo mikia yao. 11Walikuwa na malaika kutoka kwenye hilo shimo lisilo na mwisho kama mfalme wao, ambaye jina lake kwa Kiebrania ni Abadonib na kwa Kiyunani ni Apolioni.
12Ole ya kwanza imepita, bado nyingine mbili zinakuja.
Tarumbeta Ya Sita
13Malaika wa sita akaipiga tarumbeta yake, nami nikasikia sauti ikitoka katika zile pembe nne za madhabahu ya dhahabu iliyoko mbele za Mungu. 14Ile sauti ikamwambia yule malaika wa sita mwenye tarumbeta, “Wafungulie wale malaika wanne waliofungwa kwenye ule mto mkubwa Eufrati.’’ 15Basi wale malaika wanne wakafunguliwa ambao walikuwa wamewekwa tayari kwa ajili ya saa hiyo na siku hiyo na mwezi huo na mwaka huo ili wawaue theluthi ya wanadamu. 16Idadi ya majeshi wapandao farasi ilikuwa 200,000,000.
17Hivi ndivyo nilivyowaona hao farasi na wapanda farasi katika maono yangu: Wapanda farasi walivaa dirii vifuani zenye rangi ya moto na yakuti samawi na kiberiti. Vichwa vya hao farasi vilikuwa kama vichwa vya simba. Moto, moshi na kiberiti vilitoka vinywani mwao. 18Theluthi ya wanadamu wakauawa kwa maafa hayo matatu, yaani, huo moto, moshi na kiberiti, vilivyotoka kwenye vinywa vya hao farasi. 19Nguvu za hao farasi zilikuwa katika vinywa vyao na kwenye mikia yao, kwa sababu mikia
b11 Kiebrania Abadoni na kwa Kiyunani Apolioni maana yake
“Mharabu,” yaani, yeye aharibuye.
9
Ufunuo wa Yohana
9
yao ilikuwa kama nyoka. yenye vichwa ambayo waliitumia kuwadhuru watu.
20Wanadamu waliosalia, ambao hawakuuawa katika maafa hayo, bado walikataa kutubu na kuacha kumwabudu shetani na vitu walivyotengeneza kwa mikono yao wenyewe, yaani, sanamu za dhahabu, za fedha, za shaba, za mawe na za miti, ambazo haziwezi kuona, kusikia wala kutembea. 21Wala hawakutubu na kuacha matendo yao ya uuaji, uchawi, uasherati wala wizi wao.
Malaika Mwenye Kitabu Kidogo Kisha nikamwona malaika mwingine mwenye nguvu akishuka kutoka mbinguni. Alikuwa amevikwa wingu na upinde wa mvua juu ya kichwa chake. Uso wake uling'aa kama jua na miguu yake ilikuwa kama nguzo za moto. 2Mkononi mwake alikuwa ameshika kitabu kidogo kilichokuwa kimefunguliwa. Akauweka mguu wake wa kuume juu ya bahari na mguu wake wa kushoto akauweka juu ya nchi kavu. 3Naye akapiga kelele kwa sauti kuu kama simba anayenguruma. Alipopiga kelele, zile radi saba zikatoa ngurumo zake. 4Nazo zile radi saba zilipotoa ngurumo, nilitaka kuanza kuandika, lakini nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, “Yatie muhuri hayo yaliyosemwa na hizo radi saba na usiyaandike.’’
5Kisha yule malaika niliyekuwa nimemwona akiwa amesimama juu ya bahari na juu ya nchi kavu akainua mkono wake wa kuume kuelekea mbinguni. 6Naye akaapa kwa Jina la Mungu aishiye milele na milele, aliyeumba mbingu na vyote vilivyomo, dunia na vyote viijazavyo, pamoja na bahari na vyote vilivyomo ndani yake, akasema, ‘‘Hakuna kungoja tena. 7Lakini katika siku zile ambazo huyo malaika wa saba atakapokaribia kuipiga hiyo tarumbeta yake, siri ya Mungu itatimizwa, kama vile alivyowatangazia watumishi wake manabii.’’
8Ndipo ile sauti niliyokuwa nimeisikia kutoka mbinguni ikasema nami tena ikaniambia, ‘‘Nenda, chukua kile kitabu kilichofunguliwa kilichoko mkononi mwa yule malaika aliyesimama juu ya bahari na juu ya nchi kavu.’’
9Basi nikamwendea nikamwomba yule malaika anipe kile kitabu kidogo. Akaniambia, ‘‘Chukua na ukile. Kitakuwa kichungu tumboni mwako, lakini kinywani mwako kitakuwa kitamu kama asali.’’ 10Hivyo nikakichukua kile kitabu kidogo kutoka mkononi mwa yule malaika nikakila. Kilikuwa kitamu kama asali kinywani mwangu, lakini baada ya kukila, tumbo langu likatiwa uchungu. 11Kisha nikaambiwa, “Imekupasa kutoa unabii tena kuhusu makabila mengi, mataifa, lugha na wafalme.’’
Mashahidi Wawili Ndipo nikapewa mwanzi wa kupimia ulio kama fimbo, nikaambiwa, “Nenda ukapime Hekalu la Mungu pamoja na madhabahu, nawe uwahesabu wale waabuduo humo. 2Lakini usiupime ua wa nje wa Hekalu, uache, kwa sababu ua huo wamepewa watu Mataifa. Hao wataukanyagakanyaga mji mtakatifu kwa muda wa miezi arobaini na miwili. 3Nami nitawapa mashahidi wangu wawili uwezo, nao watoe unabii kwa muda wa siku 1,260, wakiwa wamevaa nguo za gunia.’’ 4Hawa ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili vya taa visimamavyo mbele za Bwana wa dunia yote. 5Kama mtu ye yote akitaka kuwadhuru, moto hutoka vinywani mwao na kuwateketeza adui zao. Hivi ndivyo mtu ye yote atakayetaka kuwadhuru atakavyokufa. 6Watu hawa wanao uwezo wa kufunga anga ili mvua isinyeshe wakati wote watakapokuwa wanatoa unabii wao. Nao watakuwa na uwezo wa kuyabadili maji kuwa damu na kuipiga dunia kwa kila aina ya mapigo mara kwa mara kama watakavyo.
7Basi watakapokuwa wamemaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika lile shimo lisilo na mwisho atapigana nao vita, atawashinda na kuwaua. 8 Maiti zao zitabaki katika barabara ya mji mkubwa, ambao kwa fumbo unaitwa Sodoma na Misri, ambapo pia Bwana wao alisulibiwa. 9Kwa muda wa siku tatu na nusu, watu wa kila kabila, jamaa, lugha na taifa wataziangalia hizo maiti zao na hawataruhusu wazikwe. 10Watu waishio duniani watazitazama kwa furaha maiti za hao manabii wawili na kushangilia kwa kupeana zawadi kwa sababu hao manabii waliwatesa watu waishio duniani.
11Lakini baada ya zile siku tatu na nusu, pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu ikawaingia, nao wakasimama kwa miguu yao na wote waliowaona wakaingiwa na hofu kuu. 12Kisha wale manabii wawili wakasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, ‘‘Njoni huku juu!’’ Nao wakapaa mbinguni katika wingu, wakati adui zao wakiwa wanawatazama.
13Saa iyo hiyo, kukatokea tetemeko kubwa la nchi na sehemu moja ya kumi ya mji
10 11
Ufunuo wa Yohana
10
ikaanguka. Watu elfu saba wakauawa katika tetemeko hilo, nao walionusurika wakaogopa sana, wakamtukuza Mungu wa mbinguni.
14Ole ya pili imekwisha kupita, tazama ole ya tatu inakuja upesi.
Tarumbeta Ya Saba
15Yule malaika wa saba akaipiga tarumbeta yake, pakawa na sauti kubwa mbinguni iliyosema :
‘‘Ufalme wa ulimwengu umekuwa
ufalme wa Bwana wetu na wa
Kristo wake,
naye atatawala milele na milele.’’
16Nao wale wazee ishirini na wanne, waliokuwa wameketi mbele za Mungu, kwenye viti vyao vya enzi wakaanguka kifudifudi wakamwabudu Mungu, 17wakisema,
‘‘Tunakushukuru, Bwana Mungu Mwenyezi,
uliyeko na uliyekuwako,
kwa kuwa umetwaa uweza Wako mkuu
na ukaanza kutawala.
18Mataifa walikasirika
kwa kuwa wakati wa ghadhabu Yako
umewadia.
Wakati umewadia wa kuwahukumu
waliokufa na kuwapa thawabu
watumishi
wako manabii na watakatifu wako
pamoja
na wale wote wanaoliheshimu Jina Lako,
wakubwa kwa wadogo na
kuwaangamiza
wale wanaoiangamiza dunia.’’
19Ndipo Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa na sanduku la agano lake likaonekana humo ndani. Kukatokea mianga ya umeme wa radi, ngurumo, sauti za radi, tetemeko la nchi na mvua kubwa ya mawe.
Mwanamke Na Joka Kukaonekana ishara kuu mbinguni: Palikuwa na mwanamke aliyevikwa jua na mwezi ukiwa chini ya miguu yake na taji ya nyota kumi na mbili ilikuwa kichwani mwake. 2Alikuwa na mimba naye akilia kwa uchungu kwa kuwa alikuwa anakaribia kuzaa. 3Kisha ishara nyingine ikaonekana mbinguni: Likaonekana joka kubwa jekundu lenye vichwa saba na pembe kumi na taji saba katika vichwa vyake. 4Mkia wake ukakokota theluthi ya nyota zote angani na kuziangusha katika nchi. Ndipo lile joka likasimama mbele ya yule mwanamke aliyekuwa karibu kuzaa ili lipate kumla huyo mtoto mara tu atakapozaliwa. 5Yule mwanamke akazaa mtoto mwanamume, atakayeyatawala mataifa yote kwa fimbo yake ya utawala ya chuma. Lakini huyo mtoto akanyakuliwa na kupelekwa kwa Mungu kwenye kiti Chake cha enzi. 6Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambako Mungu alikuwa amemtayarishia mahali ili apate kutunzwa huko kwa muda wa siku 1,260.
Malaika Mikaeli Amshinda Yule Joka
7 Basi palikuwa na vita mbinguni: Mikaeli na malaika zake wakapigana na hilo joka, nalo joka pamoja na malaika zake likapigana nao. 8Lakini joka na malaika zake wakashindwa na hapakuwa tena na nafasi kwa ajili yao mbinguni. 9Lile joka kuu likatupwa chini, yule nyoka wa zamani aitwaye Ibilisi au Shetani, aupotoshaye ulimwenguni wote. Akatupwa chini duniani, yeye pamoja na malaika zake.
Ushindi Mbinguni Watangazwa
10Kisha nikasikia sauti kuu mbinguni ikisema,
“Sasa Wokovu na uweza na Ufalme wa
Mungu wetu umekuja na mamlaka ya
Kristo wake.
Kwa kuwa ametupwa chini mshtaki wa
ndugu zetu,
anayewashtaki mbele za Mungu usiku
na mchana.
11Nao wakamshinda
kwa damu ya Mwana-Kondoo
na kwa neno la ushuhuda wao.
Wala wao hawakuyapenda maisha yao
hata kufa.
12Kwa hiyo, furahini ninyi mbingu na wote
wakaao humo!
Lakini ole wenu nchi na bahari,
kwa maana huyo Shetani ameshuka
kwenu,
akiwa amejaa ghadhabu, kwa sababu
anajua ya kuwa muda wake ni mfupi!’
13Lile joka lilipoona kuwa limetupwa chini duniani, lilimfuatilia yule mwanamke aliyekuwa amezaa mtoto mwanamume. 14Lakini huyo mwanamke akapewa mabawa mawili ya tai
12
Ufunuo wa Yohana
11
mkubwa, kusudi aweze kuruka mpaka mahali palipotayarishwa kwa ajili yake huko nyikani, ambako atatunzwa kwa wakati na nyakati na nusu wakatia ambako yule joka hawezi kufika. 15Ndipo lile joka likamwaga maji kama mto kutoka kinywani mwake, ili kumfikia huyo mwanamke na kumkumba kama mafuriko. 16Lakini nchi ikamsaidia huyo mwanamke kwa kufungua kinywa na kuumeza huo mto ambao huyo joka alikuwa ameutoa kinywani mwake. 17Kisha lile joka likapatwa na hasira kali kwa ajili ya huyo mwanamke, likaondoka ili kupigana vita na watoto waliosalia wa huyo mwanamke, yaani, wale wanaozitii amri za Mungu na kuushika ushuhuda wa Yesu Kristo. Lile joka likasimama kwenye mchanga wa bahari. 18Yule joka akajikita katika mchanga ulioko ufuoni mwa bahari.
Mnyama Kutoka Baharini Nami nikamwona mnyama akitoka ndani ya bahari. Mnyama huyo alikuwa na pembe kumi na vichwa saba, akiwa na taji kumi kwenye hizo pembe zake na juu ya kila kichwa kulikuwa na jina la kukufuru. 2Mnyama yule niliyemwona alikuwa kama chui, miguu yake ilikuwa kama ya dubu na kichwa chake kama cha simba. Lile joka likampa huyo mnyama nguvu zake, kiti chake cha enzi na mamlaka makubwa. 3Kimojawapo ya vichwa vya huyo mnyama kilikuwa kama kilichokwisha kupata jeraha la mauti, lakini jeraha hilo la mauti likapona. Ulimwengu wote ukashangaa ukamfuata huyo mnyama. 4Watu wakaliabudu lile joka kwa sababu lilikuwa limempa huyo mnyama mamlaka yake, pia wakamwabudu huyo mnyama na kuuliza, “Ni nani aliye kama huyu mnyama? Ni nani awezaye kupigana vita naye?’’
5Huyo mnyama akapewa kusema maneno ya kujisifu na kukufuru na kutumia mamlaka yake kwa muda wa miezi arobaini na miwili. 6Akafungua kinywa chake ili kumkukufuru Mungu, akilitukana Jina lake na mahali aishipo na wale wakaao mbinguni. 7Pia akaruhusiwa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda. Akapewa uwezo juu ya watu wa kila kabila, jamaa, lugha na taifa. 8Nao watu wote waishio duniani watamwabudu huyo mnyama, yaani, wale wote ambao majina yao hayakuandikwa
a14 “Wakati na nyakati na nusu wakati” hapa maana yake ni miaka
mitatu na nusu. kwenye kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo aliyechinjwa tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
9“Yeye aliye na sikio na asikie.
10Ikiwa mtu ni wa kuchukuliwa mateka,
atachukuliwa mateka.
Ikiwa mtu ni wa kuuawa kwa upanga,
atauawa kwa upanga.
Hapa ndipo penye wito kwa ajili ya saburi na imani ya watakatifu.
Mnyama Kutoka Katika Dunia
11Kisha nikamwona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika dunia. Alikuwa na pembe mbili kama mwana-kondoo, lakini akanena kama joka. 12Akatumia mamlaka yote ya yule mnyama wa kwanza kwa niaba yake, naye akawafanya wote wakaao duniani kumwabudu yule mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona. 13Huyu mnyama wa pili akafanya ishara kuu na za ajabu, hata kusababisha moto kushuka toka mbinguni kuja duniani watu wakiona waziwazi. 14Kwa sababu ya zile ishara alizokuwa amepewa uwezo wa kufanya kwa niaba ya yule mnyama wa kwanza, akawadanganya wakaao duniani. Akawaamuru wasimamishe sanamu kwa heshima ya yule mnyama aliyekuwa amejeruhiwa kwa upanga lakini akaishi. 15Akapewa uwezo wa kuipa pumzi ile sanamu ya yule mnyama wa kwanza, ili iweze kusema na kuwasababisha wale wote waliokataa kuiabudu hiyo sanamu kuuawa. 16Pia alimlazimisha kila mmoja, mdogo na mkubwa, tajiri na maskini, mtu huru na mtumwa, atiwe chapa kwenye mkono wake wa kuume au kwenye kipaji chake cha uso, 17ili kwamba mtu ye yote asiweze kununua wala kuuza isipokuwa amekuwa na hiyo chapa, ambayo ni jina la huyo mnyama au tarakimu za jina lake.
18Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili na ahesabu tarakimu za huyo mnyama, kwa maana ni tarakimu za kibinadamu. Tarakimu zake ni 666.
Mwana-Kondoo Na Wale 144,000 Kisha nikatazama na hapo mbele yangu alikuwepo Mwana-Kondoo, akiwa amesimama juu ya Mlima Sayuni. Pamoja naye walikuwa wale watu 144,000 wenye Jina la Mwana-Kondoo na Jina la Baba Yake likiwa limeandikwa kwenye vipaji vya nyuso zao. 2Nami nikasikia sauti kutoka mbinguni kama
13 14
Ufunuo wa Yohana
12
sauti ya maji mengi yaendayo kasi na sauti kama ngurumo ya radi. Sauti hiyo niliyoisikia ilikuwa kama sauti ya wapiga vinubi wakipiga vinubi vyao. 3Nao wakaimba wimbo mpya mbele ya hicho kiti cha enzi na mbele ya wale viumbe wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne. Hakuna mtu ye yote aliyeweza kujifunza wimbo huo isipokuwa hao watu 144,000 waliokuwa wamekombolewa kutoka duniani. 4Hawa ndio wale ambao hawakujitia unajisi kwa wanawake, kwa kuwa wao ni mabikira. Wao humfuata Mwana-Kondoo kila aendako. Hawa wamekombolewa kutoka miongoni mwa wanadamu wakawa malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo. 5Vinywani mwao hapakuonekana uongo, wala hawakuwa na hatia yo yote.
Malaika Watatu
6Kisha nikamwona malaika mwingine akiruka juu angani, naye alikuwa na Injili ya milele ya kuwatangazia wale waishio duniani, yaani, kwa kila taifa, kabila, lugha na jamaa. 7Akasema kwa sauti kubwa, ‘‘Mcheni Mungu na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imewadia. Mwabuduni Yeye aliyeziumba mbingu, dunia, bahari na chemchemi za maji.’’
8Malaika wa pili akafuata akisema, “Ameanguka! Ameanguka Babeli aliye mkuu, yeye aliyeyafanya mataifa yote kulewa kwa mvinyo wa ghadhabu ya uasherati wake.’’
9Malaika wa tatu akawafuata hao wawili akisema kwa sauti kubwa, “Kama mtu ye yote anamwabudu huyo mnyama na sanamu yake na kutiwa chapa yake kwenye kipaji chake cha uso au kwenye mkono wake, 10yeye naye, atakunywa mvinyo wa hasira kali ya Mungu ambayo imemiminwa katika kikombe cha ghadhabu yake pasipo kuchanganywa na maji. Naye atateswa kwa moto uwakao na kiberiti mbele ya malaika watakatifu na mbele za Mwana-Kondoo. 11Nao Moshi wa mateso yao hupanda juu milele na milele. Hakuna mapumziko, mchana wala usiku, kwa wale wamwabuduo huyo mnyama na sanamu yake, au kwa ye yote anayepokea chapa ya jina lake.’’ 12Hapa ndipo penye subira na uvumilivu wa watakatifu, yaani, wale wanaozishika amri za Mungu na kudumu kuwa waaminifu kwa Yesu.
13Kisha nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, “Andika: Wamebarikiwa wale wafao katika Bwana tangu sasa.”
“Naam,’’ asema Roho, “watapumzika kutoka katika taabu zao, kwa kuwa matendo yao yatawafuata.’’
Kuvuna Mavuno Ya Dunia
14Nikatazama, hapo mbele yangu palikuwa na wingu jeupe na aliyekuwa ameketi juu ya hilo wingu alikuwa kama Mwana wa Adamu, mwenye taji ya dhahabu kichwani mwake na mundu mkali mkononi mwake. 15Kisha malaika mwingine akaja kutoka Hekaluni naye akamwita kwa sauti kubwa yule aliyekuwa ameketi juu ya lile wingu akasema, “Chukua mundu wako ukavune kwa kuwa wakati wa mavuno umewadia, kwa maana mavuno ya dunia yamekomaa.’’ 16Hivyo yule aliyekuwa ameketi juu ya lile wingu akauzungusha mundu wake duniani, nayo dunia ikavunwa.
17Malaika mwingine akatoka katika Hekalu lililoko mbinguni, naye pia alikuwa na mundu mkali.
18Kisha malaika mwingine, aliyekuwa na mamlaka juu ya moto, akatoka kwenye madhabahu, naye akamwita yule malaika mwenye mundu mkali kwa sauti kubwa, akisema, “Chukua mundu wako mkali ukakusanye vichala vya mizabibu ya dunia, maana zabibu zake zimeiva.’’ 19Hivyo yule malaika akauzungusha mundu wake duniani na kukusanya vichala vya zabibu za dunia na kuzitupa kwenye shinikizo kubwa la ghadhabu ya Mungu. 20Lile shinikizo likakanyagwa nje ya mji, nayo damu ikatiririka kama mafuriko kutoka katika hilo shinikizo kufikia kimo cha hatamu za farasia, kwa umbali wa maili mia mbili.b
Malaika Saba Na Mapigo Saba Ndipo nikaona ishara nyingine kubwa ya ajabu mbinguni, malaika saba wenye yale mapigo saba ya mwisho, kwa sababu kwa mapigo hayo ghadhabu ya Mungu ilikuwa imekamilika. 2Nikaona kile kilichoonekana kama bahari ya kioo iliyochanganyikana na moto. Kando ya hiyo bahari, walikuwa wamesimama wale watu waliomshinda yule mnyama na sanamu yake pamoja na tarakimu ya jina lake. Mikononi mwao walikuwa wameshika vinubi walivyopewa na Mungu. 3Nao wakaimba wimbo wa Mose, mtumishi wa Mungu na wimbo wa Mwana-Kondoo wakisema:
a20 Kimo cha hatamu za farasi hapa ni kama mita moja na nusu
(1.5m)
b20 Maili 200 hapa ni sawa na kilomita 320 15
Ufunuo wa Yohana
13
“Bwana Mungu Mwenyezi, matendo Yako ni
makuu na ya ajabu Mfalme wa zamani
zote,
njia Zako Wewe ni za haki na za kweli!
4Ni nani ambaye hatakuogopa Wewe Bwana na
kulitukuza Jina Lako?
Kwa kuwa Wewe peke yako ndiwe
mtakatifu.
Mataifa yote yatakuja na kuabudu mbele
zako,
kwa kuwa matendo yako ya haki
yamedhihirishwa.’’
5Baada ya haya nikatazama, nalo hekalu la hema la ushuhuda lilikuwa limefunguliwa mbinguni, 6ndani ya lile hekalu wakatoka malaika saba wakiwa na mapigo saba. Walikuwa wamevaa nguo safi za kitani ing’aayo na kufungwa mikanda ya dhahabu vifuani mwao. 7Ndipo mmoja wa wale wenye uhai wanne akawapa wale malaika saba mabakuli saba ya dhahabu yaliyojaa ghadhabu ya Mungu, Yeye aishiye milele na milele. 8Nalo lile hekalu lilijawa na moshi uliotokana na utukufu wa Mungu na uweza wake, wala hakuna ye yote aliyeweza kuingia mle hekaluni mpaka yale mapigo saba ya wale malaika saba yalipomalizika.
Mabakuli Saba Ya Ghadhabu Ya Mungu Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka mle hekaluni ikiwaambia wale malaika saba, “Nendeni, mkayamwage duniani hayo mabakuli saba ya ghadhabu ya Mungu.’’
2Malaika wa kwanza akaenda akalimwaga hilo bakuli lake juu ya nchi. Majipu mabaya yenye maumivu makali yakawapata wale watu wote waliokuwa na chapa ya yule mnyama na kuiabudu sanamu yake.
3Malaika wa pili akalimwaga bakuli lake baharini, nayo ikabadilika kuwa damu kama ya mtu aliyekufa na kila kiumbe hai kilichokuwa ndani ya bahari kikafa.
4Malaika wa tatu akalimwaga bakuli lake katika mito na chemchemi za maji, nazo zikawa damu. 5Ndipo nikamsikia malaika msimamizi wa maji akisema,
“Wewe una haki katika hukumu hizi
ulizotoa,
wewe uliyeko, uliyekuwako, uliye
Mtakatifu,
kwa sababu umehukumu hivyo,
6kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu
Wako na manabii Wako,
nawe umewapa damu wanywe kama
walivyostahili.’’
7Nikasikia madhabahu ikiitikia,
“Naam, Bwana Mungu Mwenyezi,
hukumu Zako ni kweli na haki.”
8Malaika wa nne akamimina bakuli lake kwenye jua, nalo likapewa nguvu za kuwaunguza watu kwa moto. 9Watu wakaunguzwa na hilo joto kali, lakini wakalaani Jina la Mungu, aliyekuwa na uwezo juu ya mapigo haya, wala hawakutubu na kumtukuza Mungu.
10Malaika wa tano akamimina bakuli lake kwenye kiti cha enzi cha yule mnyama, nao ufalme wake ukagubikwa na giza. Watu wakatafuna ndimi zao kwa ajili ya maumivu 11wakamlaani Mungu wa mbinguni kwa sababu ya maumivu na majeraha yao, wala hawakutubu kwa ajili ya matendo yao maovu.
12Malaika wa sita akamimina bakuli lake kwenye mto mkubwa Eufrati, maji yake yakakauka ili kutayarisha njia kwa ajili ya wafalme watokao mashariki. 13Kisha nikaona roho wachafu watatu waliofanana na vyura wakitoka katika kinywa cha lile joka na katika kinywa cha yule mnyama na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. 14Hizo ndizo roho za pepo wachafu zitendazo miujiza. Nazo huwaendea wafalme wa ulimwengu wote na kuwakusanya tayari kwa ajili ya vita katika siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.
15“Tazama, naja kama mwivi! Amebarikiwa yeye akeshaye na kuziweka tayari nguo zake ili asiende uchi na kuoenekana aibu yake”.
16Ndipo wakawakusanya wafalme pamoja mahali paitwapo “Armagedoni’’a kwa Kiebrania.
17Malaika wa saba akamimina bakuli lake angani na sauti kubwa ikatoka mle hekaluni katika kile kiti cha enzi, ikisema, ‘‘Imekwisha kuwa!’’ 18Kukawa na mianga ya umeme wa radi, ngurumo, radi na tetemeko kubwa la ardhi. Hapajawa kamwe na tetemeko la ardhi kama hilo tangu mwanadamu awepo duniani, hivyo lilikuwa tetemeko kubwa ajabu. 19Ule mji mkubwa ukagawanyika katika sehemu tatu, nayo miji ya mataifa ikaanguka. Mungu
a16 Armagedoni au Har-magedoni hapa ina maana mlima
Magido mahali pa kinabii ambapo wafalme wote wa dunia
watakusanyika kwa vita katika siku ya Mungu Mwenyezi.
16
Ufunuo wa Yohana
14
akaukumbuka Babeli ule uliokuwa mkuu na kuupa kikombe cha hasira na ghadhabu Yake. 20Kila kisiwa kikatoweka wala milima haikuonekana. 21Mvua kubwa ya mawe, mawe yenye uzito wa talanta mojab yakaanguka kutoka mbinguni, yakawaangukia wanadamu. Nao wanadamu wakamlaani Mungu kwa ajili ya hayo mapigo ya mvua ya mawe, kwa sababu pigo hilo lilikuwa la kutisha. Kahaba Mkuu Na Mnyama
Mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na yale mabakuli saba akaja akaniambia, ‘‘Njoo, nitakuonyesha adhabu ya yule kahaba mkuu, aketiye juu ya maji mengi. 2Yule ambaye wafalme wa dunia walizini naye na watu wakaao duniani walilewa kwa mvinyo wa uzinzi wake.’’
3Kisha yule malaika akanichukua katika Roho akanipeleka nyikani. Huko nikamwona mwanamke mmoja ameketi juu ya mnyama mwekundu aliyejaa majina ya kumkufuru Mungu mwili mzima. Mnyama huyo alikuwa na vichwa saba na pembe kumi. 4Huyo mwanamke alikuwa amevaa mavazi ya rangi ya zambarau na nyekundu, akimetameta kwa dhahabu, vito vya thamani na lulu. Mkononi mwake alikuwa ameshika kikombe cha dhahabu kilichojaa mambo ya machukizo na uchafu wa uzinzi wake. 5Kwenye kipaji chake cha uso palikuwa pameandikwa jina:
“SIRI,
BABELI MKUU,
MAMA WA MAKAHABA
NA MACHUKIZO YA DUNIA.’’
6Nikaona kuwa huyo mwanamke alikuwa amelewa kwa damu ya watakatifu, yaani, damu ya wale watu waliouawa kwa ushuhuda wa Yesu.
Nilipomwona huyo mwanamke, nilistaajabu sana. 7Ndipo yule malaika akaniambia, ‘‘Kwa nini unastaajabu? Nitakufafanulia siri ya huyo mwanamke na huyo mnyama aliyempanda, mwenye vichwa saba na pembe kumi. 8Huyo mnyama, ambaye ulimwona, wakati fulani alikuwepo, lakini sasa hayupo, naye atapanda kutoka katika lile shimo lisilo na mwisho na kwenda kwenye maangamizo. Watu waishio duniani ambao majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha uzima tangu kuumbwa kwa
b21 Talanta moja ni kama kilo 34 ulimwengu watastaajabu kumwona huyo mnyama, kwa maana alikuwepo, wakati fulani na sasa hayupo, lakini atakuja.
9‘‘Hapa ndipo penye akili pamoja na hekima. Vile vichwa saba ni vilima saba ambavyo huyo mwanamke amevikalia. 10Pia hivyo vichwa saba ni wafalme saba ambao miongoni mwao watano wamekwisha kuanguka, mwingine hajaja bado, lakini atakapokuja, atalazimika kukaa kwa muda mfupi. 11Yule mnyama aliyekuwepo wakati fulani na ambaye sasa hayupo, yeye ni mfalme wa nane. Ni miongoni mwa wale saba, naye anakwenda kwenye maangamizi.
12‘‘Zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi ambao bado hawajapokea ufalme, lakini ambao watapokea mamlaka kuwa wafalme kwa wakati mmoja pamoja na yule mnyama. 13Hawa wana nia moja, nao watamwachia yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao. 14Watafanya vita na Mwana-Kondoo, lakini Mwana-Kondoo atawashinda kwa sababu Yeye ni Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme. Yeye atakuwa pamoja na watu wake walioitwa ambao ni wateule wake na wafuasi wake waaminifu.’’
15Kisha yule malaika akaniambia, ‘‘Yale maji uliyoyaona, yule kahaba akiwa ameketi juu yake ni jamaa za watu, makutano, mataifa na lugha. 16Zile pembe kumi ulizoziona, pamoja na huyo mnyama, watamchukia huyo kahaba, watamfilisi na kumwacha uchi, watamla nyama yake na kumteketeza kwa moto. 17Kwa maana Mungu ataweka mioyoni mwao kutimiza kusudi lake kwa kukubali kumpa yule mnyama mamlaka yao ya utawala mpaka maneno ya Mungu yatakapotimia. 18Yule mwanamke uliyemwona ni ule mji mkubwa unaotawala juu ya wafalme wa dunia.’’ Kuanguka Kwa Babeli
Baada ya haya nikaona malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni, akiwa na mamlaka makuu na dunia ikamulikiwa na mng’ao wake. 2Naye akalia kwa nguvu kwa sauti kubwa, akisema:
‘‘Umeanguka! Umeanguka Babeli ulio
mkuu!
Umekuwa makao ya mashetani
na makazi ya kila pepo mchafu,
makazi ya kila ndege na kila mnyama
achukizaye.
3Kwa maana mataifa yote yamekunywa mvinyo
17 18
Ufunuo wa Yohana
15
wa uasherati wake,
nao wafalme wa dunia wamefanya uzinzi
naye,
nao wafanyi biashara wa dunia
wametajirika
kutokana na wingi wa utajiri wake.’’
4Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema:
“Tokeni katikati yake, enyi watu wangu,
ili msije mkashiriki dhambi zake,
ili usije ukapatwa na pigo lake lo lote,
5kwa kuwa dhambi zake zimelundikana hadi
mbinguni,
naye Mungu ameukumbuka uhalifu wake.
6Mtendee kama yeye alivyotenda,
umlipe mara mbili kwa ajili ya yale
aliyotenda.
Katika kikombe chake mchanganyie mara
mbili ya kile alichochanganya.
7Mpatie mateso na huzuni nyingi sawa na
utukufu na anasa alizojipatia.
Kwa kuwa moyoni mwake hujivuna
akisema,
‘Mimi ninatawala kama malkia,
mimi si mjane wala sitaona huzuni
kamwe.’
8Kwa hiyo mapigo yatampata kwa siku moja:
mauti, maombolezo na njaa.
Naye atateketezwa kwa moto, kwa maana
amhukumuye ni Bwana Mungu
Mwenyezi.
9“Wafalme wa dunia waliozini naye na kushiriki anasa zake watakapoona moshi wa kuungua kwake, watamlilia na kumwombolezea. 10Watasimama mbali na kulia kwa hofu kutokana na mateso yake na kusema:
“ ‘Ole! Ole Ee mji mkuu,
Ee Babeli mji wenye nguvu!
Hukumu yako imekuja katika saa moja!’
11“Na wafanyi biashara wa duniani wanalia na kuomboleza kwa sababu hakuna anunuaye bidhaa zao tena. 12Bidhaa za dhahabu, za fedha, za vito vya thamani na vya lulu, kitani safi, nguo za rangi ya zambarau, hariri, nguo nyekundu, aina zote za miti ya manukato, vifaa vyote vya pembe za ndovu, vifaa vyote vya miti yenye thamani kuliko yote, shaba nyeusi, chuma na marmar, 13mdalasini, vikolezi, uvumba, manemane, uvumba wenye harufu nzuri, divai, mafuta ya zeituni, unga mzuri na ngano, ng'ombe na kondoo, farasi na magari, watumwa, pia na roho za wanadamu.
14‘‘Watasema, ‘Yale matunda ambayo roho yako iliyatamani yamekoma. Utajiri wako wote na fahari yako vimetoweka, wala haviwezi kupatikana tena kamwe!’ 15Wale wafanyibiashara wauzao bidhaa hizo na kupata utajiri wao kutoka kwake watasimama mbali naye kwa hofu ya mateso yanayompata. Watalia na kuomboleza wakipiga kelele wakisema:
16‘‘ ‘Ole! Ole, Ee, mji mkubwa,
uliyekuwa umevikwa mavazi ya kitani
safi, ya rangi ya zambarau na
nyekundu,
ukimetameta kwa dhahabu, vito vya
thamani na lulu!
17Katika muda wa saa moja utajiri wote mkubwa
kama huu umeangamia!’
‘‘Kila nahodha, mabaharia wote wasafirio baharini na wote wafanyao kazi melini watasimama mbali naye. 18Watakapoona moshi wa kuungua kwake watalia wakisema, ‘Je, ulipata kuwako mji mkuu kama huu?’ 19Nao watajirushia mavumbi vichwani mwao huku wakilia na kuomboleza wakisema:
‘‘ ‘Ole, Ole, Ee mji mkubwa,
mji ambao wote wenye meli baharini
walitajirika kwa kupitia mali zako!
Katika saa moja tu umeangamizwa!
20Furahia uharibifu wake, Ee mbingu!
Furahini ninyi watakatifu na mitume na
manabii!
Kwa kuwa Mungu ameutendea kama vile
ulivyowatendea ninyi.’ ’’
21Kisha malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe kubwa kama la kusagia akalitupa baharini akisema:
“Hivyo ndivyo mji mkubwa Babeli
utakavyotupwa chini
kwa nguvu wala hautaonekana tena.
22Nyimbo za wapiga vinubi na waimbaji, wapiga
filimbi na sauti za wapiga tarumbeta
hazitasikika ndani yako tena.
Ndani yako kamwe hataonekana fundi
mwenye ujuzi wa aina yo yote.
Ufunuo wa Yohana
16
Wala sauti ya jiwe la kusagia
kamwe haitaisikika.
23Mwanga wa taa
hautaangaza tena ndani yako.
Wala sauti ya bwana arusi na bibi arusi
kamwe haitasikiwa ndani yako.
Kwa kuwa wafanyi biashara wako walikuwa
watu maarufu wa dunia
na mataifa yote yalidanganyika kwa
uchawi wako.
24Ndani yako ilionekana damu ya manabii na ya
watakatifu
na watu wote waliouawa duniani.’’ Shangwe Huko Mbinguni
Baada ya haya nikasikia sauti kama sauti ya umati mkubwa wa watu mbinguni ikisema kwa nguvu :
“Haleluya!
Wokovu na utukufu na uweza
ni vya Mungu wetu,
2kwa maana hukumu Zake ni za kweli na za
haki.
Amemhukumu yule kahaba mkuu
aliyeuharibu ulimwengu kwa uzinzi
wake.
Mungu amemlipiza kisasi kwa ajili ya damu
ya watumishi wake.’’
3Wakasema tena kwa nguvu:
“Haleluya!
Moshi wake huyo kahaba unapanda juu
milele na milele.’’
4Wale wazee ishirini na wanne pamoja na wale viumbe wenye uhai wanne wakaanguka kifudifudi, wakamwabudu Mungu, aliyekuwa ameketi kwenye kile kiti cha enzi. Wakasema kwa sauti kuu:
‘‘Amen! Haleluya!’’
5Kisha sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi, ikisema:
‘‘Msifuni Mungu wetu,
ninyi watumishi wake wote,
ninyi nyote mnaomcha,
wadogo kwa wakubwa!’’
6Kisha nikasikia sauti kama sauti ya umati mkubwa wa watu, kama sauti ya maji mengi yaendayo kasi na kama ngurumo kubwa ya radi ikisema:
‘‘Haleluya!
Kwa maana Bwana Mungu wetu
Mwenyezi anamiliki.
7Tufurahi, tushangilie
na kumpa utukufu!
Kwa maana arusi ya Mwana-Kondoo
Imewadia,
na bibi arusi wake amejiweka tayari.
8Akapewa kitani safi, nyeupe inayong'aa
ili avae.’’
(Hiyo kitani safi inawakilisha matendo ya haki ya watakatifu.)
9Ndipo yule malaika akaniambia, “Andika haya: ‘Wamebarikiwa wale walioalikwa kwenye karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo !’ ’’ Naye akaongeza kusema, “Haya ndiyo maneno ya kweli ya Mungu.’’
10Ndipo nikaanguka kifudifudi miguuni pake ili kumwabudu, lakini yeye akaniambia, “Usifanye hivyo! Mimi pia ni mtumishi mwenzako pamoja na ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Mwabudu Mungu! Maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii.’’
Aliyepanda Farasi Mweupe
11Kisha nikaona mbingu imefunguka na hapo mbele yangu akiwepo farasi mweupe, ambaye Yeye aliyempanda huyo farasi aliitwa Mwaminifu na wa Kweli. Yeye ahukumu kwa haki na kupigana vita. 12Macho yake ni kama miali ya moto na juu ya kichwa Chake kuna taji nyingi. Alikuwa na jina lililoandikwa ambalo hakuna mtu ye yote anayelijua isipokuwa Yeye mwenyewe. 13Alikuwa amevaa vazi lililochovywa kwenye damu na Jina lake ni ‘‘Neno la Mungu.’’ 14Majeshi ya mbinguni walikuwa wakimfuata, wakiwa wamepanda farasi weupe, hali wamevaa mavazi ya kitani nzuri, nyeupe safi. 15Kinywani mwake mlitoka upanga mkali ambao kwa huo atayaangusha mataifa. Atayatawala kwa ‘‘fimbo yake ya utawala ya chuma.’’ Atalikanyaga shinikizo la mvinyo wa ghadhabu ya Mungu Mwenyezi. 16Kwenye vazi lake na paja lake liliandikwa jina hili:
MFALME WA WAFALME NA BWANA WA
MABWANA.
19
Ufunuo wa Yohana
17
Mnyama Na Majeshi Yake Yashindwa
17Nami nikamwona malaika amesimama ndani kwenye jua, akaita ndege wote warukao angani kwa sauti kuu, ‘‘Njoni, kusanyikeni kwa ajili ya karamu kubwa ya Mungu, 18ili mpate kula nyama ya wafalme na ya majemadari, ya mashujaa, ya farasi na ya wapanda farasi, nyama ya wanadamu wote walio huru na watumwa, wadogo na wakubwa.’’
19Kisha nikamwona yule mnyama na wafalme wa dunia pamoja na majeshi yao wakiwa wamekusanyika pamoja ili kupigana vita dhidi ya yulealiyempanda huyo farasi mweupe pamoja na jeshi Lake.20Lakini yule mnyama akakamatwa pamoja na huyo nabii wa uongo ambaye alikuwa amefanya ishara kwa niaba ya huyo mnyama, ambaye kwa ishara hizi aliwadanganya wale waliopokea chapa ya huyo mnyama na kuiabudu sanamu yake. Hawa wawili wakatupwa wakiwa hai ndani ya ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti. 21Wale waliosalia waliuawa kwa upanga uliotoka kinywani mwa yule aliyekuwa amempanda huyo farasi mweupe, nao ndege wote wakajishibisha kwa nyama yao.
Utawala Wa Miaka Elfu Moja Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, akiwa ameshika ufunguo wa lile shimo lisilo na mwisho na mnyororo mkubwa mkononi mwake. 2Akalishika lile joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ndiye Ibilisi na Shetani, naye akamfunga kwa muda wa miaka 1,000. 3Akamtupa katika lile shimo lisilo na mwisho, akamfunga humo na kulitia lakiri, ili kumzuia asiendelee kudanganya mataifa mpaka hiyo miaka 1,000 itimie. Baada ya hayo atafunguliwa kwa muda mfupi.
4Kisha nikaona viti vya enzi vilivyokuwa vimekaliwa na hao waliopewa mamlaka ya kuhukumu. Nami nikaona roho za wale waliokatwa vichwa kwa sababu ya ushuhuda wa Yesu na kwa sababu ya neno la Mungu. Hawakuwa wamemsujudia huyo mnyama wala sanamu yake wala hawakupokea ile chapa yake kwenye vipaji vya nyuso zao au kwenye mikono yao. Wakawa hai na kutawala pamoja na Kristo miaka 1,000. 5(Wafu waliosalia hawakufufuka mpaka ilipotimia hiyo miaka 1,000.) Huu ndio ufufuo wa kwanza. 6Wamebarikiwa tena ni watakatifu wale walio na sehemu katika huo ufufuo wa kwanza.Hao mauti ya pili haina nguvu juu yao, bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye kwa muda wa miaka 1,000.
Kuhukumiwa Kwa Shetani
7Hiyo miaka 1,000 itakapotimia, Shetani atafunguliwa kutoka kifungoni mwake, 8naye atatoka ili kuyadanganya mataifa yaliyopo katika pembe nne za dunia, yaani, Gogu na Magogu apate kuwakusanya tayari kwa vita. Idadi yao ni kama mchanga ulioko Pwani. 9Nao walitembea katika eneo lote la dunia, wakaizunguka kambi ya watakatifu na ule mji uliopendwa. Lakini moto ukashuka kutoka mbinguni na kuwateketeza. 10Naye Ibilisi aliyewadanganya akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti alipo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao wakateswa huko mchana na usiku, milele na milele.
Wafu Wanahukumiwa
11Kisha nikaona kiti kikubwa cha enzi cheupe, dunia na mbingu zikaukimbia uso wake Yeye aliyeketi juu yake, wala mahali pao hapakuonekana. 12Nami nikawaona wafu wakubwa na wadogo, wakiwa wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi na vitabu vikafunguliwa. Pia kitabu kingine kikafunguliwa ambacho ni cha uzima. Hao wafu wakahukumiwa sawasawa na matendo yao kama yaliyoandikwa ndani ya hivyo vitabu. 13Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake, nayo mauti na kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Kila mtu akahukumiwa kulingana na yale aliyotenda. 14Kisha Mauti na Kuzimu zikatupwa katika ziwa la moto. Hii ndio Mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. 15Iwapo mtu jina lake halikuonekana katika kile kitabu cha uzima, alitupwa ndani ya lile ziwa la moto.
Mbingu Mpya Na Nchi Mpya Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya, maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapakuwepo na bahari tena. 2Nikaona Mji Mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, ukiwa umeandaliwa kama bibi arusi aliyepambwa kwa ajili ya mumewe. 3Nami nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, ‘‘Tazama, makao ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atakaa pamoja nao. Yeye atakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wake, naye Mungu mwenyewe
20 21
Ufunuo wa Yohana
18
atakuwa pamoja nao. 4Atafuta kila chozi, kutoka katika macho yao. Mauti haitakuwepo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu, kwa maana mambo ya kwanza yamekwisha kupita.’’
5Naye yule aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi akasema, ‘‘Tazama, nayafanya mambo yote kuwa mapya.’’ Pia akasema, “Andika haya, maana maneno haya ni ya kuaminika tena ni kweli.’’
6Akaniambia, “Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Yeye aonaye kiu nitampa kunywa kutoka katika chemchemi ya maji ya uzima bila gharama yo yote. 7Yeye atakayeshinda atayarithi haya yote, Nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu. 8Lakini waoga, wasioamini, wachafu, wauaji, wazinzi, wachawi, waabudu sanamu, pamoja na waongo wote, mahali pao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.’’
9Kisha mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na yale mabakuli saba ya hayo mapigo saba ya mwisho akaja akaniambia, ‘‘Njoo, nami nitakuonyesha bibi arusi, yaani, mke wa Mwana-Kondoo.’’ 10Naye akanichukua katika Roho hadi kwenye mlima mkubwa na mrefu, akanionyesha ule Mji Mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu. 11Ulikuwa uking'aa kwa utukufu wa Mungu kama kito chenye thamani sana, kama yaspi, safi kama kioo. 12Ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu wenye malango kumi na mawili, pakiwa na malaika kumi na wawili kwenye hayo malango. Kwenye malango hayo yaliandikwa majina ya yale makabila kumi na mawili ya Israeli. 13Kulikuwa na malango matatu upande wa mashariki, matatu upande wa kaskazini, matatu upande wa kusini na matatu upande wa magharibi. 14Ukuta wa huo mji ulikuwa na misingi kumi na miwili na juu yake yaliandikwa majina ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo.
15Huyo malaika aliyesema nami alikuwa na ufito wa dhahabu wa kupimia huo mji, malango yake na kuta zake. 16Mji huo ulikuwa mraba, urefu wake ulikuwa sawa na upana. Akaupima huo mji kwa huo ufito akaukuta una kama kilometa 2,400a urefu wake na upana wake na kwenda juu kwake vilikuwa sawa. 17Akaupima ukuta wake, ulikuwa na unene wa dhiraa 144b
a16 Kilomita 2,400 hapa ni sawa na maili 1,500
b17 Dhiraa 144 ni sawa na mita 64.8 yaani karibu Km. 65. kwa kipimo cha kibinadamu ambacho huyo malaika alikuwa akikitumia. 18Ukuta huo ulijengwa kwa yaspi hali mji wenyewe ulijengwa kwa dhahabu safi, iking'aa kama kioo. 19Misingi ya mji huo ilipambwa kwa kila aina ya kito cha thamani. Msingi wa kwanza ulikuwa wa yaspi, wa pili yakuti samawi, wa tatu kalkedoni, wa nne zamaridi, 20wa tano sardoniki, wa sita akiki, wa saba krisolitho, wa nane zabarajadi, wa tisa yakuti manjano, wa kumi krisopraso, wa kumi na moja hiakintho, wa kumi na mbili amethisto. 21Yale malango kumi na mbili yalikuwa ni lulu kumi na mbili, kila lango lilikuwa limetengenezwa kwa lulu moja. Barabara za mji huo zilikuwa za dhahabu safi ing'aayo kama kioo.
22Sikuona Hekalu ndani ya huo mji kwa sababu Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo ndio Hekalu lake. 23Ule mji hauhitaji jua wala mwezi kuuangazia kwa sababu utukufu wa Mungu ndio nuru yake na Mwana-Kondoo ndiye taa yake. 24Mataifa yatatembea yakiangaziwa na nuru yake na wafalme wa duniani wataleta fahari yao ndani yake. 25Malango yake hayatafungwa kamwe mchana, kwa maana hakutakuwa na usiku humo. 26Utukufu na heshima za mataifa zitaletwa humo. 27Lakini kitu kichafu hakitaingia humo kamwe, wala mtu ye yote atendaye mambo ya aibu au ya udanganyifu. Bali watakaoingia humo ni wale tu ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.
Mto Wa Maji Ya Uzima Kisha yule malaika akanionyesha mto wa maji ya uzima, maangavu kama kioo yakitiririka kutoka kwenye kile kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo, 2kupitia katikati ya barabara kuu ya huo mji. Kwenye kila upande wa huo mto kulikuwa na mti wa uzima utoao matunda ya aina kumi na mbili, ukizaa matunda yake kila mwezi. Nayo majani ya mti huo ni kwa ajili ya uponyaji wa mataifa. 3Katika mji huo hakutakuwa tena na kitu cho chote kilicholaaniwa, bali kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kitakuwamo humo na watumishi wake watamtumikia, 4nao watamwona uso Wake na Jina lake litakuwa kwenye vipaji vya nyuso zao. 5Usiku hautakuwako tena, wala hawatahitaji mwanga wa taa au wa jua, kwa maana Bwana Mungu atakuwa nuru yao, nao watatawala milele na milele. 22
Ufunuo wa Yohana
19
6Kisha yule malaika akaniambia, “Maneno haya ni ya kuaminika na kweli. Bwana, Mungu wa roho za manabii, amemtuma malaika wake kuwaonyesha watumishi wake yale ambayo hayana budi kutukia upesi.
Bwana Yesu Anakuja
7‘‘Tazama, naja upesi! Amebarikiwa yeye ayashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki.’’
8Mimi Yohana, ndiye niliyesikia na kuyaona mambo haya. Nami nilipokwisha kuyasikia na kuyaona, nilianguka chini nikasujudu miguuni pa yule malaika aliyekuwa akinionyesha mambo hayo. 9Lakini yeye akaniambia, “Usifanye hivyo! Mimi ni mtumishi pamoja nawe na ndugu zako manabii na wote wanaoyashika maneno ya kitabu hiki. Msujudie Mungu!’’
10Kisha akaniambia, “Usiyafunge maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, kwa sababu wakati umekaribia. 11Atendaye mabaya na aendelee kutenda mabaya, aliye mchafu na aendelee kuwa mchafu, yeye atendaye haki na aendelee kutenda haki na yeye aliye mtakatifu na aendelee kuwa mtakatifu.’’
12“Tazama, naja upesi! nikiwa na mshahara wangu, nami nitamlipa kila mtu sawasawa na alivyotenda. 13Mimi ni Alfa na Omega, wa Kwanza na wa Mwisho, Mwanzo na Mwisho.
14“Wamebarikiwa wale wafuao nguo zao, ili wapate haki ya kuuendea huo mti wa uzima na kuuingia huo mji kwa kupitia kwenye malango yake. 15Huko nje wako mbwa, wachawi, wazinzi, wauaji, waabuduo sanamu na kila mtu apendaye udanganyifu na kuufanya.
16“Mimi Yesu, nimemtuma malaika wangu kushuhudia mambo haya kwa ajili ya makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile Nyota ya asubuhi ing'aayo.’’
17Roho na bibi arusi wanasema, “Njoo!’’ Naye asikiaye na aseme, “Njoo!’’ Ye yote mwenye kiu na aje na kila anayetaka na anywe maji ya uzima bure.
18Namwonya kila mtu asikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki: Mtu ye yote akiongeza cho chote, Mungu atamwongezea mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. 19Kama mtu ye yote akipunguza cho chote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.
20Yeye anayeshuhudia mambo haya asema, “Naam, naja upesi!’’
Amen. Njoo Bwana Yesu.
21Neema ya Bwana Yesu iwe na watakatifu wote. Amen.
Ufunuo wa Yohana
20
Labels:
Mjue mungu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WELCOME TO THE GREAT BROTHERHOOD.
ReplyDeleteDo you want to be a member of Illuminati as a brotherhood
that will make you rich and famous in the world and have
power to control people in the high place in the worldwide
.Are you a business man or woman,artist, political,
musician, student, do you want to be rich, famous, powerful
in life, join the Illuminati brotherhood cult today and get
instant rich sum of. 2 million dollars in a week, and a free
home.any where you choose to live in this world
BENEFITS GIVEN TO NEW MEMBERS of ILLUMINATI.
1. A Cash Reward of USD $500,000 USD
2. A New Sleek Dream CAR valued at USD $300,000 USD
3.A Dream House bought in the country of your own choice
4. One Month holiday (fully paid) to your dream tourist
destination.
5.One year Golf Membership package
6.A V.I.P treatment in all Airports in the World 7.A total
Lifestyle change 8.Access to Bohemian Grove
account every month as a member
9.One Month booked Appointment with Top 5 world
Leaders and Top 5 Celebrities in the World.
If you are interested of joining us in the great brotherhood of illuminati CONTACT MR ROLAND or WhatsApp him +2348155285233
or email:illuminatipower666brotherhood@gmail.com